Saturday, April 18

ARI-Tumbi Kuendesha Mafunzo juu ya utoaji wa huduma kwa wakulima

Kituo cha utafiti kanda ya magharibi ARI - Tumbi kinatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa watafiti wake juu ya utoaji huduma kwa wakulima yenye lengo la kuongeza ufanisi katika kueneza teknolojia sahihi kwa wadau wake.

Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo nchini -ASDP. Lengo hasa ni kuwafanya watafiti wawe na mtazamo mpya ambao unalenga kutoa huduma zaidi na kuwa na mfumo shirikishi katika kufanya utafiti au kueneza teknolojia sahihi. vile mafunzo yanalenga kuhimiza ushirikishwaji wa wadau wengine hasa watoa huduma na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) ili kuweza kufikia walengwa kwa urahisi na kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali. Mafunzo haya yatatolewa kwa awamu tano ambazo zitahusisha nadharia (wiki 1) na vitendo (mwezi 1). Mwishoni mwa kila awamu, watafiti wataleta mrejesho (feedback) na kuanisha changamoto zilizopo kwa ajili ya kuzifanyia kazi.
Matarajio ya mafunzo haya ni kuweza kubadilisha mtazamo hasa hali ya sasa ya utoaji huduma ambazo msistizo ni kumuchukulia mkulima kama mteja na mshirika katika kupambana na umaskini. Pia ni kumjengea uwezo mtafiti hasa katika kufanya taftishi ambazo zitaleta tija. Mafunzo haya yataratibiwa na wataalamu walioteuliwa na wizara za Kilimo Chakula na Ushirika na Mifugo na Uvuvi.

words of wisdom

"Without food security there wont be time for positive innovation"

Search This Blog

Powered By Blogger